3.Wazo la ubunifu linaendana na dhamira yako, kwa nini unataka kufuga kuku, je nafsi yako inahisia na hicho unachokiwaza? Au umefurahishwa na fulani anavyo fuga! Ni vyema kwanza ukaifanya nafsi yako ipende wazo lako la ubunifu, kisha ufikirie unataka kuwa nani katika sekta ya kuku either uwe mfugaji wa kuku wa mayai, uwe mfugaji wa kuku wa nyama, au uwe mfugaji wa kuku wa asili ambao unatumia kwa nyama na mayai, hapo watu wengi wanajiweka katika wakati mgumu sana na kushindwa kufanya maamuzi sahihi.
Cha msingi chakufanya unapofikiria kufuga kuku wa biashara gani lazima uingalie watu unaowalenga kuwauzia, je unayo nertwork yakutosha(kujuana na walaji) je unasoko umelipata sehemu?
Usianze kufuga kuku wa nyama kama huna mtu wakukusaidia wakati wakutafuta soko au kama hauna soko kabisa, utaingia hasara kwa kuku kukaa muda murefu na kula mtaji wako.
JE KUKU WA AINA GANI WANAFAIDA ZAIDI?
Ndugu msomaji kwanza tutambue kuna miradi ya aina mbili
1. Miradi ya mda mfupi(short term project) hapa namaanisha kuku wa nyama(broiler)
2. Miradi ya muda mrefu(long term project) hapa namaanisha kuku wa mayai(layers) na kuku wa asili(chotara na kienyeji)
faida inategemeana na mzunguko wako wa kibiashara na uwezo ulionao wakutoa bidhaa nzuri na kwa uwingi, unapowekeza biashara ya muda murefu ukianza kuvuna faida unavuna kwa muda mrefu na ni kila siku unakuwa na bidhaa kwenye biashara yako ukilinganisha na ya muda mfupi, kuku wa aina zote wanafaida kutegemeana na mazingira yakibiashara uliyonayo.
Dhamira yako pia iambatane na uvumilivu kwa sababu kuna matatizo mengi yanatokea katika mradi huu wa ufugaji kutokana unahusika na vitu vyenye uhai ambavyo mauti kwake ni lazima wanatofautia muda tu wakufa,ingawa vifo vingi sisi wenye mifugo hiyo tunahusika tukiwa makini tunauwezo wa kuzuia..
Itaendelea.....
Itaendelea.....
No comments:
Post a Comment