MUDA MZURI WA KUNUNUA VIFARANGA.
Watu wengi tumekuwa tunaingia hasara kubwa sana pasipo kujua, mtu anakopa pesa milioni kadhaa anaagiza vifaranga wa layers, broiler au chotara wengine na baadae wale vifaranga wanakufa kwa wingi sana.mtu anaweza agiza vifaranga wa layers 300 mwisho wa siku wanabakia 150 too bad, na mwingine anaweza agiza 1000 wakabakia 200 tu.
Na wakati mwingine wanaisha kabisa wote.
muda wakuagiza vifaranga
Muda mzuri ni muda ambao wewe mwenye idea/mwenye wazo/hamasa/ mwenye uchungu uko free yaani hauko bise au hauko kazini, Muda ambao uko likizo, au muda ambao una off za kutosha.
Muda huu ni mzuri sana kwa wewe sasa kuingiza vifaranga na kama una likizo ya siku 28 maana yake hapa ni wiki 4 vifaranga wanakuwa tayari wamesimama na wanaweza jisaidia au kufanya baadhi ya mambo wenyewe.
Makosa tunayo fanya:
- Kuagiza vifaranga na kumwachia House boy avitazame
- Kuagia vifaranga na kumuachia House girl kazi ya kulisha na kutunza
-Kuagiza na kumuachia mtu ambaye hana hobby na kuku,
Epuka haya
- Kumuachia vifaranga mtu asiye kuwa na hobby, mtu ambaye kwake kinyesi cha kuku ni sawa na cha binadamu ni kosa kubwa sana kumuachia mtu wa ina hii
- Kuanza kulea vifaranga kwa simu hili ni kosa kubwa mno, vifaranga hawaltunzwi kwa njia ya simu kamwe na usijaribu.
Vifaranga siku zao za mwanzo wanahitaji care ya kiwango cha juu kabisa, na uangalizi wa kutosha na some time unashauriwa kuhamishia makazi bandani yaani unaweka kiti kabisa bandani au pembeni ya bruda ya vifaranga.
Madhara ya kuingiza vifaranga bandani na kuachia watu wengine;
- Kuanza kulaumu walio kuuzia vifaranga-Hapa sasa lawama huenda kwa alie uza vifaranga oo kaniuzia vifaranga vigonjwa, kaniuzia vifaranga dhaifu, lawama huwa nyingi sana kukwepa lawama kuu.Hakikisha unakuwa incharge wa kutunza vifaranga kwa ngalau wiki 4 za mwanzo, ingawa hata baada ya hapo sio tiketi ya sasa kuanza kuwatunza kwa simu....
No comments:
Post a Comment