>Saklama ndugu zangu wafugaji,Leo napenda niwakukumbushe muoshe vyombo vya maji kila unapoweka maji yakunywa ya kuku,kama kuku wako wako unaweza wapa maji mara 7 kwa siku basi osha vyombo mara 7 kwa sabuni yenye antbacteria,vyombo vya chakula osha kwa wiki mara tatu tenga ratiba ya siku yakuosha vyombo hivyo.
>jitahidi banda kuwa safi mda wote ili kutokua na bacteria ndani,fanya usafi wa mala kwa mala...
MTUNZE KUKU SASA AKUTUNZE BAADAE...
ARUSHA KUKU FARM
Ufugaji ni maisha
Friday, April 14, 2017
Thursday, March 23, 2017
MDA MZURI WAKUAGIZA VIFARANGA.
MUDA MZURI WA KUNUNUA VIFARANGA.
Watu wengi tumekuwa tunaingia hasara kubwa sana pasipo kujua, mtu anakopa pesa milioni kadhaa anaagiza vifaranga wa layers, broiler au chotara wengine na baadae wale vifaranga wanakufa kwa wingi sana.mtu anaweza agiza vifaranga wa layers 300 mwisho wa siku wanabakia 150 too bad, na mwingine anaweza agiza 1000 wakabakia 200 tu.
Na wakati mwingine wanaisha kabisa wote.
muda wakuagiza vifaranga
Muda mzuri ni muda ambao wewe mwenye idea/mwenye wazo/hamasa/ mwenye uchungu uko free yaani hauko bise au hauko kazini, Muda ambao uko likizo, au muda ambao una off za kutosha.
Muda huu ni mzuri sana kwa wewe sasa kuingiza vifaranga na kama una likizo ya siku 28 maana yake hapa ni wiki 4 vifaranga wanakuwa tayari wamesimama na wanaweza jisaidia au kufanya baadhi ya mambo wenyewe.
Makosa tunayo fanya:
- Kuagiza vifaranga na kumwachia House boy avitazame
- Kuagia vifaranga na kumuachia House girl kazi ya kulisha na kutunza
-Kuagiza na kumuachia mtu ambaye hana hobby na kuku,
Epuka haya
- Kumuachia vifaranga mtu asiye kuwa na hobby, mtu ambaye kwake kinyesi cha kuku ni sawa na cha binadamu ni kosa kubwa sana kumuachia mtu wa ina hii
- Kuanza kulea vifaranga kwa simu hili ni kosa kubwa mno, vifaranga hawaltunzwi kwa njia ya simu kamwe na usijaribu.
Vifaranga siku zao za mwanzo wanahitaji care ya kiwango cha juu kabisa, na uangalizi wa kutosha na some time unashauriwa kuhamishia makazi bandani yaani unaweka kiti kabisa bandani au pembeni ya bruda ya vifaranga.
Madhara ya kuingiza vifaranga bandani na kuachia watu wengine;
- Kuanza kulaumu walio kuuzia vifaranga-Hapa sasa lawama huenda kwa alie uza vifaranga oo kaniuzia vifaranga vigonjwa, kaniuzia vifaranga dhaifu, lawama huwa nyingi sana kukwepa lawama kuu.Hakikisha unakuwa incharge wa kutunza vifaranga kwa ngalau wiki 4 za mwanzo, ingawa hata baada ya hapo sio tiketi ya sasa kuanza kuwatunza kwa simu....

Saturday, February 25, 2017
SIFA ZA MAYAI KUATAMIWA.
- yawe masafi(yafutwe na kitambaa laini na maji ya vuguvugu)
- yasiwe na nyufa ya nje au ya ndani
- yasiwe na mviringo kama mpira au ncha kali
- yasiwe na siku nyingi zaidi ya siku9
- yasiwe yaliyohifadhiwa sehemu yenye joto
- yahifadhiwe sehemu yenye hewa ya kutosha
- NB:mayai yahifadhiwe ncha au sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu
- yai lenye mbegu ndani huweza kutambulika au kuonekana kuanzia siku ya 8 hadi 10,viashiria vyake huwa ni yai kuonesha mishipa au mizizi ndani pamoja na kiini cheusi.
Thursday, January 19, 2017
NJIA ZA KUANZISHA MRADI WA KUKU
SEHEM YA PILI
3.Wazo la ubunifu linaendana na dhamira yako, kwa nini unataka kufuga kuku, je nafsi yako inahisia na hicho unachokiwaza? Au umefurahishwa na fulani anavyo fuga! Ni vyema kwanza ukaifanya nafsi yako ipende wazo lako la ubunifu, kisha ufikirie unataka kuwa nani katika sekta ya kuku either uwe mfugaji wa kuku wa mayai, uwe mfugaji wa kuku wa nyama, au uwe mfugaji wa kuku wa asili ambao unatumia kwa nyama na mayai, hapo watu wengi wanajiweka katika wakati mgumu sana na kushindwa kufanya maamuzi sahihi.
Cha msingi chakufanya unapofikiria kufuga kuku wa biashara gani lazima uingalie watu unaowalenga kuwauzia, je unayo nertwork yakutosha(kujuana na walaji) je unasoko umelipata sehemu?
Usianze kufuga kuku wa nyama kama huna mtu wakukusaidia wakati wakutafuta soko au kama hauna soko kabisa, utaingia hasara kwa kuku kukaa muda murefu na kula mtaji wako.
JE KUKU WA AINA GANI WANAFAIDA ZAIDI?
Ndugu msomaji kwanza tutambue kuna miradi ya aina mbili
1. Miradi ya mda mfupi(short term project) hapa namaanisha kuku wa nyama(broiler)
2. Miradi ya muda mrefu(long term project) hapa namaanisha kuku wa mayai(layers) na kuku wa asili(chotara na kienyeji)
faida inategemeana na mzunguko wako wa kibiashara na uwezo ulionao wakutoa bidhaa nzuri na kwa uwingi, unapowekeza biashara ya muda murefu ukianza kuvuna faida unavuna kwa muda mrefu na ni kila siku unakuwa na bidhaa kwenye biashara yako ukilinganisha na ya muda mfupi, kuku wa aina zote wanafaida kutegemeana na mazingira yakibiashara uliyonayo.
Dhamira yako pia iambatane na uvumilivu kwa sababu kuna matatizo mengi yanatokea katika mradi huu wa ufugaji kutokana unahusika na vitu vyenye uhai ambavyo mauti kwake ni lazima wanatofautia muda tu wakufa,ingawa vifo vingi sisi wenye mifugo hiyo tunahusika tukiwa makini tunauwezo wa kuzuia..
Itaendelea.....
Itaendelea.....
NJIA ZA KUANZISHA MRADI WA KUKU
SEHEM YA KWANZA.
1.kwanza fahamu vitu vya msingi unavyotakiwa kuwa navyo
ambavyo ni
=wazo la ubunifu
=dhamira (unafuga kwa lengo gani)
=eneo la kufugia
=aina ya kuku unaotaka kufuga
=mtaji
=usikivu
=elimu ya ufugaji wa kuku
=kufuga kisasa/kufuga kibiashara
hizo ni baadhi tu ya vigezo muhimu =
2.Anza kidogo uwezavyo( mtaji)
watu wengi wanashindwa kuendesha miradi hii wakihofia uwezo wakuweza kuhudumia, sio lazima uwe na pesa nyingi ndipo uanze kufuga kuku, au sio lazima uanze na kuku wengi kwa kutimiza ndoto zako, neno la msingi wewe mwenye mtaji mdogo anza kidogo uwezavyo, hii itakuongezea juhudi yakufikia malengo yako.
tambua ujasilia mali wowote unahuitaji kuku, huwezi kukimbilia hatua ya tatu wakati hatua ya kwanza hujaifanya, pale utakapo anza na kidogo utaweza kukua vyema na kuwa ujuzi mkubwa wakuhimili mikikimikiki ya ufugaji ambayo kama ungeanza kwa pupa ungeweza kushindwa kuendesha mradi wako.
Itaendelea..................

Wednesday, January 4, 2017
UMHIMU WA VIOTA KATIKA BANDA
1. Humshawishi kuku kutaga
2. Hupunguza kupotea kwa mayai ovyo.
3. Hupunguza idadi ya mayai kuvunjika
4. Huzuia ulaji wa mayai.
5. Hurahisisha uokotaji wa mayai.
6. Mayai huwa safi na salama
7. Huongeza makusanyo/idadi ya maya
2. Hupunguza kupotea kwa mayai ovyo.
3. Hupunguza idadi ya mayai kuvunjika
4. Huzuia ulaji wa mayai.
5. Hurahisisha uokotaji wa mayai.
6. Mayai huwa safi na salama
7. Huongeza makusanyo/idadi ya maya
![]() |

SIFA ZA JOGOO NA MITETEA YA KIENYEJI
Sifa za kuzingatia wakati wa kuchagua mitetea:
Wawe na:
1:Umbile kubwa.
2:Uwezo wa kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 6).
3:Uwezo wa kustahimili magonjwa.
4:Uwezo wa kukua haraka.
5;Uwezo wa kutaga mayai mengi {zaidi ya 15 kwa mtago mmoja (
clutch)
6:Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi na kuwalea.
Sifa za
kuzingatia wakati wa kuchagua majogoo
Jogoo bora, awe na:
1:Umbo kubwa.
2:Miguu imara na yenye nguvu.
3:Kucha fupi.
4:Mwenye nguvu.
5:Machachari.
6:Upanga/kilemba kikubwa.
7:Uwezo wa kuitia chakula mitetea.
Tabia ya kupenda vifaranga
ATHARI ZA UPUNGUFU WA VIRUTUBISHO KWENYE CHAKULA.
1:Kudumaa
2:Kupungua uzito,
3:Kulemaa viungo
4:Kuvunjika mifupa kwa urahisi
5:Kutaga mayai yenye ganda laini
6:Kutaga mayai machache
7:Kutoota manyoya yakutosha.
8:unyonyoka na kujikunja manyoya.
9:Kujaa kwa tumbo
TIBA
Athari zinazotokana na upungufu wa
virutubishi zinaweza kurekebishwa kwa
kuwapa kuku virutubishi vilivyopungua
katika chakula.
KINGA
Kuwalisha chakula kilicho na
mchanganyiko wenye uwiano sahihi
katika wanga, protini, vitamini, madini
na maji ya kutoshabo.![]() |
Kuku aliekosa chakula chenye virutubisho vya kutosha. Kuku waliopata chakula chenye virutubisho vya kutosha. |
Subscribe to:
Posts (Atom)